Monday, November 4, 2013
January Makamba:Natafakari urais 2015
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba, amesema anatafakari iwapo awanie urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na hii ni kutokana na kuwepo kwa watu wengi hasa ndani ya CCM wanaomtaka kugombea nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi.
Makamba ambae pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM alisema: “Kwanza ni kweli kwamba kuna ushawishi kuhusu suala hilo kutoka kwa vijana walioko nje na ndani ya chama, wanataaluma, baadhi ya wazee na watu wengine iwe kwa makundi au mtu mmoja mmoja wamekuwa wakinishawishi kugombea kwa muda sasa.”
source:millardayo.com
Labels:
Kitaifa:siasa
No comments:
Post a Comment