Saturday, October 12, 2013
Ushauri wa Bure kwa wanaojiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma.
kwanza kabisa niwapongeze kwa kufanikiwa kuwa sehemu ya wateule ambao wanajiunga na chuo kikuu cha Dodoma,bila shaka ni wengi wangependa nafasi hiyo waipate lakini bahati haikuwa yao
pengine wengine wakapelekwa vyuo vingine wasivyovipenda.Lakini pia natambua kasumba iliyomtaani ambayo kwa sasa naamini ukweli na uongo ni kama maji na mafuta kwani maneno mengi ya mtaani yamekuwa yanakifanya chuo kikuu cha Dodoma kionekane kama hakifai kusoma lakini sasa wengi wao waliowadadisi wametambua kukosea.waliobaki ni wale wabishi wasio na ufahamu wa mambo halisi,kwa kifupi changamoto zipo ambazo kwa kiasi kikubwa zipo vyuo vyote vya Tanzania.kwa hiyo dhana yangu ni kwamba umechaguliwa kusoma UDOM au chuo kikuu kingine chochote Tanzania,fuatilia mambo muhimu ya kuyajua ili angalau usiache lengo lako.
1.wahi kufika chuo
bila shaka kupitia mtandao umepata 'joining instruction' inayokuelekeza mambo mengi ikiwemo tarehe ya kufunguliwa chuo hasa kwa nyie mwaka wa kwanza.kwa bahati nzuri au mbaya mnaishi na wanafunzi wenzenu waliotangulia,mnapotaka kujua umuhimu wa kuwahi chuo wengi wao hujaribu kupotosha kwa kuwaaminisha kwamba hakuna haja.Lakini mimi nakwambia leo fika mapema ili upate kujua mambo mengi kabla masoma hayajaanza,hiyo itakusaidia kupunguza maswali mengi ambayo yangekuumiza kichwa.kwa mfano utapata kufahamu mazingira ya chuo,walimu wako,majengo utakayokuwa unakuwa kwa majina,mali pa kupata msaada pindi unapokutana na tatizo,utamjua mkuu wa 'college' unayosoma ,muundo wa kiutawala kutoka ngazi za juu mpaka chini kwa majina na vyeo vyao.Na mengine mengi utakutana nayo,nakuhakikishia hutajuta kamwe kuwahi kufika chuo.
2.sheria za chuo
katika hili unapaswa kuwa makini nalo sana,kwani ndio sehemu ya mkataba wa wewe kuendelea kuwepo chuoni.kumbuka msemo wa kisheria huu"kutokujua sheria hakukupi dhamana ya wewe kufanya makosa".hii inamaana kwamba sheria haitambui kama wewe hujui sheria,kwa pale chuo unaweza ona malengo yako yanaishia kurudi nyumbani baada ya kufanya makosa ya kufukuzwa chuo.Zingatia sana hili nakusihi
3.andaa fedha ya kutosha ya kujikimu ukiwa chuoni
kuna wengine hapa wanaweza kwenda chuo kwa kutegemea mkopo wakiamini kwamba ukifika tu na hela inaingia kwenye akaunti.labda nikutahadharishe kwa hili,huwezi pata pesa kabla taarifa zako hazijafika bodi ya mkopo kutoka chuo mara baada ya kuripoti.kwa kawaida fedha huingia kwenye akaunti ndani ya wiki moja na nusu mpaka mbili kutegemeana nawahasibu watakavyoamua,kwa hiyo kama huna hela na kumbuka muda huo wote ni wageni hamfahamiani kwa hiyo hamuwezi kuazimana chochote,ndugu yangu utapata tabu.ukiwa na hela utaelekezwa sehemu ya kula chakula japo pia kuna sehemu maarufu kama kwa wajasi"wajasiriamali" ambako wengi hupunguza bajeti huko kwani angalau bei ni elfu moja kwa sahani chakula chenye mixer kibao hahahaa! nenda kahakikishe au kula wali maharage cafeteria.
4.soma kwa bidii
katika hili nipende kusema tu utumie ule msemo wa biashara asubuhi,ili kama ni ngumu ujue ujipange vipi maana mtajiona kama mko loose sana siku za mwanzo,lakini utata huja pindi test zikianza na hali umelimbikiza masomo,bila shaka huo utakuwa mwanzo wa kupunguza kujiamini hivyo kushindwa kufikia malengo yako kwani masomo yatakushinda sana.ukijipanga vizuri utafurahia sana maisha ya chuo.kumbuka kuna maneno maarufu sana vyuoni Ku-sap(SUPPLIMENTARY) maana yake kurudia somo husika,ku-disco(DISCONTINUE) Kufeli na kurudi nyumbani bila kelele na ku-kerry(Carrying)yaani kusoma tena somo husika mwaka wa masomo unaofuata.Yote haya yanakupata kama hujajiandaa vizuri,hii ndiyo sababu kubwa.
5.ukimwi pia huku upo.
kwa sasahivi hatuna budi kupeana ukweli,mahubiri yamekuwa mengi mahali popote juu ya ugonjwa wa ukimwi,hata huku utakutana na matangazo kama hayo,mafundisho pia.jitahidi kuwa mwangalifu usijekuwa mfano lakini endelea kuwaombea ambao wameshaupata kwa sababu haujui waliupataje.
Bila shaka nimegusa baadhi ya yale niliyopenda nikushirikishe.natumaini ramani nzuma utakuwa unaifahamu ili ufike University of Dodoma(UDOM) kama hutambui,ukifikika stenti kuu utatakiwa kwenda kituo cha daladala kinaitwa jamatini,ukifika hapo utakuta daladala nyingi lakini wewe utaeleke upande gari za UDOM zinapaki uliza konda yeyote juu ya gari ipi upande kuelekea 'college' utakayosoma.ukifika mapema nauli haizidi tsh 500 na mizigo pia utalipia kama umejifungasha sana,Usihofu utapeli si sana ila kuwa makini usije tapeliwa.
Haya,nikutakie masomo mema ndani ya Dodoma katika chuo kikuu cha Dodoma(UDOM)
Labels:
Habari Vyuoni
No comments:
Post a Comment