Wednesday, December 25, 2013

salamu za krismas na mwaka mpya toka kwa TOPNewz!!


Wapendwa watanzania wenzangu,wote kwa ujumla bila kujali dini au dhehebu, nawapongeza kwa kuwa sehemu ya wateule wa Mungu katika kuwa sehemu ya wote waliofurahia siku ya leo.japo kuna baadhi kutokana na imani zao hii si siku kuu kwao lakini kutokana na utamaduni wetu sisi binadamu kuungana pamoja katika sikukuu hizi  ni faraja yangu kwamba wote tumeguswa na sikukuu hii.

Kwa kawaida sikukuu huwa ni njema tangu kuandaliwa kwake, japokuwa kutokana na ubunifu wetu sisi wengi wetu katika kuiboresha hujikuta tunazidisha na hatimaye tunaifanya siku ya kutenda dhambi.Ukitaka kukubaliana na mimi jaribu kufuatilia matangazo mengi yaliyopo au chunguza nyumba za kulala wageni na wenyeji majibu yake ni uthibitisho tosha,kwa kifupi ni kwamba matangazo mengi yatahusu kwa lugha ya kileo wanaita "sehemu za kula bata" ambapo disko ndo kitu cha msingi hapo,ndiyooo disko si  baya lakini disko lenye mambo mengi yanayokuwa kinyume na matarajio,mabinti kuvaa kasoro uchi,pombe kuwa sehemu ya furaha na mengineyo mengi.
Kwa mtazamo wa TOPNewz!!  tunaamini kwamba siku kama hizi za sikukuu kama ni ya kidini ni siku muhimu sana kutafakari uhusiano wako na Mungu wako unayemwamini na kuweza kuangalia jinsi ya kurekebisha ili hata kwako mwenyewe ujipe asilimia katika kuzingatia yale unayo amini.
kama ni sikukuu za kufunga mwaka TOPNewz tunaamini kwamba ni sikukuu zinazotoa nafasi kutafakari jinsi mwaka ulivyo kamilika na kuangalia kama malengo uliyojiwekea yamefikiwa na kuweza kupanga malengo mapya yatakayo kufanye uithamini kila siku inayoitwa leo.
Zaidi ya yote TOPNewz tunaamini,kitu muhimu zaidi kwa binadamu ni upendo na furaha,hivyo hakikisha siku kama hii haiharibiwi kwa lolote na kukufanya uboreke bali iwe mwanzo wa furaha iliyopotea na chumvi au sukari kwa furaha iliyopo japo vitu hiv visizidishwe!!
Nimengi ya kukumbushana japo unaweza shiriki kukumbusha kwa kuandika katika sehemu ya maoni hapo chini.TOPNewz inawatakia AMANI na FURAHA pia UPENDO katika kipindi chote hiki cha  SIKUKUU ya KRISMASI na MWAKA MPYA!!

No comments:

Post a Comment

google +

google +
chris kyando

FIND US ON FACEBOOK