Mgombea wa uraisi kwa tiketi ya CHADEMA Edward Lowassa
amewataka wananchi wa Ngaramtoni Arusha wamchague ili aweze kumaliza kero zao
mapema mara baada ya kuingia Ikulu.
“Nipeni madaraka tarehe 25 niwaonyeshe kazi” alisema
Lowassa.
Edward Lowasa ameendelea kufanya kampeni za lala salama huku
akisisitiza vipaumbele vya serikali yake mara atakapo pata idhini ya wananchi
kuongoza nchi.
“Nitashughurikia tatizo la Elimu na Afya nchini kwani elimu
ni chanzo cha mafanikio ya mambo mengine”.alisema Lowassa.
Hata hivyo wananchi katika mkutano katika uwanja wa Mringa
walipaza sauti wakimwambia kwa sauti “Maji” “Umeme” naye akasisitiza wampe madaraka tarehe 25 ili
awashughulikie wale ambao hawawajibiki kutatua matatizo ya wananchi.
Ameendelea kuwaahidi walimu na wakulima kuwa maisha yao
yatabadilika kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi wao na kuahidi serikali
kutokuwa chanzo cha migogoro na matatizo.
No comments:
Post a Comment