Amou hadji mzaliwa wa Iran amepamba vichwa vya habari wiki
hii kwa kuvunja rekodi ya mtu ambaye
hajaoga kwa muda mrefu iliyokuwa
ikishikiliwa na Mhindi Kailash Sigh ambaye hakuwahi kuoga kwa zaidi ya miaka
38.Bwana Amou Hadji alioga kwa mara ya mwisho mwaka 1954 akiwa na miaka 20 tu ,baada
ya hapo hajaoga tena.
Inasemekana bwana
Hadji alikuwa na msongo wa mawazo sana ujana wake akaamua kuishi maisha ya
kujitenga na jamii.Alifanikiwa kuwakwepa vijana ambao walijitolea kumwogesha
mara nyingi kwani aliamini usafi kwake ungemsababishia kuumwa!
Muda wote huo alipenda kula vyakula na vinywaji visivyokuwa katika
hali ya usafi na kuvuta kinyesi cha
wanyama kama sigara kutumia kiko chake.
No comments:
Post a Comment