Saturday, October 17, 2015

Ratiba ligi kuu uingereza leo jumamosi ya tar 17/10/2015


kocha wa Chelsea Jose Mourinho akiwa kazini



Ratiba ya mechi zitazochezwa leo jumamosi EPL ni kama ilivyo hapa katika jedwali:
mpaka sasa club ya manchester city inaongoza baada ya mechi nane zilizochezwa kama inavyoonesha katika msimamo hapa chini unaoonesha club 10 za mwanzo .
Liverpool baada ya kumtimua kocha wao Brendan Rodgers na kumpa mikoba kocha mpya Jugen Klopp watakuwa na kibarua kigumu ugenini dhidi ya watoto wa mjini Totenham hotspurs huku macho ya wengi ikiwa ni kuona jinsi gani kocha mpya ambaye wachambuzi wanasema anakuja na hamasa mpya katika ligi inayofuatiliwa kwa karibu na wadau wengi duniani ataanza kazi ya kuwainua mashabiki wa Liverpool na kuanza kutembea kifua mbele.
msimamo ya timu 10 za mwanzo ni kama ulivyo hapa chini:

Darajani pia kutakuwa na kazi ngumu kwa timu ya Chelsea ambayo inanolewa na kocha asiyeishiwa maneno Jose Mourinho pale chelsea itakapowakaribisha Aston Vila ambao kama leo ingekuwa ndo mwisho wa ligi basi wangeweza shuka daraja kwani wako nafasi ya 18 katika msimamo huku chelsea wakiwa nafasi ya 16.Matoke mabaya kwa chelsea leo yataongeza uwezekano wa mmiliki wa timu bilionea Roman Abromovich kumtimua kocha Jose Mourinho licha ya kumpatia mkataba mpya mapema kabla ligi kuanza.
ikumbukwe Mourinho amefungiwa kutohudumu kama kocha mechi moja na shilikisho la mpira la uingereza FA baada ya kukutwa na kosa la kukiuka sheria zilizowekwa  alipokuwa akitoa maoni yake baada ya chelsea kufungwa 3 kwa 1 na Southampton.
msimamo wa timu 10 za mwisho ni kama unavyoonekana hapa chini.

No comments:

Post a Comment

google +

google +
chris kyando

FIND US ON FACEBOOK