wema na diamond wakicheza pamoja Leaders Club
Kwa kawaida binadamu wengi hupendezwa na kufanya kitu ambacho unakipenda kwa wakati fulani bila kujali wengine wanamtazamo gani juu ya kitu hicho.Lakini mara nyingine pia wengine hufanya kitu ambacho wengine wanapenda kukisikia,hii inatokea sana kwa mastaa hasa wa mziki.
Mfano mzuri upo kwa mahusiano ya CHRIS BROWN na aliyekuwa mpenzi wake RIHANNA,kutokana na yaliyotokea ya chris kumpiga rihanna na kuhukumiwa na mahakama,wengi walitaka kujua nini kitafuata baada ya Chris kumaliza adhabu aliyopewa ya kufanya usafi ikizingatiwa pia alitakiwa kuwa mbali na Rihanna.mara kwa mara kamera ziliwabamba pamoja na hata kauli zao juu ya mahusiano yao ziliongeza mvuto kwa wanahabari kufuatilia.
Sasa kwetu hapa bongo,ukimtaja kijana Diamond,basi lazima stori ya Wema iingia kiasi kwamba hata wao wamegundua uhusiano wao ni njia tosha ya kuvuta hadhira kuwajadili wao.mfano safari ya Dubai ambayo inahusu utengenezaji filamu itakayo wahusisha wao,na mengine mengi zaidi ni pale viwanja vya Leaders Club ambapo Diamond alifanya show na bila kutarajia Wema naye kupanda baada ya kuitwa na diamond na kucheza naye'ukimwona'. angalia picha hapa chini
Kama unadhani unalolote la ku 'share' basi usisite kuchangia kwa kuandika katika comment hapa chini.
No comments:
Post a Comment