kwa kawaida watu wengi wanaotumia pombe wanaelewa sana ninapozungumzia
‘hang'over’.kwa ambao hawatambui hii ni
ile hali ya mtu kujisikia mchovu,kichwa kuuma na hali nyingine nyingi za kukera
mara baada ya kuamka iwapo usiku wa jana
uliutumia kwa kunywa pombe hasa kwa kiwango kikubwa.
kutokana na hali hiyo watu wengi wamekuwa wakitumia njia mbalimbali ili kurudisha hali yao kuwa ya kawaida,wengine hutumia supu na maji kwa wingi,wengine huamini kunywa tena pombe wakiamini dawa ya moto ni moto na nyinginezo.
watafiti wa china wamegundua katika utafiti wao
kwamba soda aina ya sprite inaweza kuwa ni chaguo bora zaidi kutibu tatizo la “hangover”.wao
waliangalia chanzo cha mtu kupata matatizo mara baada ya kulewa
pombe.wakafuatilia mchakato mzima jinsi mwili unavyofanya kazi kwa mtu akinywa
pombe,wakagundua kwamba kimeng’enya kiitwacho kitaalamu Alcohol Dehydrogenase(ADH)
hubadili kimea cha pombe kuwa “Acetaldehyde”
ambayo inaaminika kuwa ndiyo chanzo cha matatizo yatokanayo na kunywa pombe
ambayo hudumu kwa muda mrefu pamoja na “hang'over”. Pia kimeng’enya kiitwacho
kitaalamu Aldehyde Dehydrogenase(ALDH) hugeuza Acetaldehyde
kuwa Acetate ambayo inaaminika kuwa
in chanzo cha faida zitokanazo na kunywa pombe.
katika utafiti wao walitumia vinywaji tofauti 57
vikijumuisha chai na vinywaji
vilivyotengenezwa kwa kuchanganywa na
madini ya kaboneti ambapo soda ya
sprite ni mojawapo.katika vinywaji hivyo walilinganisha jinsi ADH
na ALDH zinavyofanya kazi.wakaona kwamba kila
kinywaji kina madhara tofauti kikiwa kwenye ADH na ALDH huku
vinywaji vingi vikionekana kuchochea ADH
kufanya kazi ambayo hupelekea matokeo mabaya baada ya kunya pombe huku
vikikandamiza utendaji kazi wa ALDH,lakini
sprite(inayojulikana kwa jina la Xue bi
huko China) ilionekana kuongeza
utendaji kazi wa ALDH huku ikikandamiza utendaji kazi wa ADH na hivyo kupunguza madhara yatokanayo na kunywa pombe.
kwa maoni yangu,kwa wale ambao wamekuwa wakisumbuliwa na
hali hiyo ni vyema wakajaribu kutumia utafiti huu pengine unaweza kuwarudisha
katika ubora wao katika utendaji wa kazi hasa ukizingatia watu wengi hasa
wanaotumia pombe siku ya jumapili hujikuta wakishindwa kufanya kazi zao
kiufanisi siku ya jumatatu.pia kama unadhani kuna njia nyingine bora waweza
kuacha ujumbe wako hapo chini.Sishauri mtu yeyote kunywa pombe,lakini ukiwa mtumiaji, huu ni ushauri wangu.
No comments:
Post a Comment